Skip to main contentAccess keys helpA-Z index
BBCSwahili.com
Maziwa Makuu
Kisomali
Arabik
Kifaransa kwa Afrika
Turqisht
 
Mara ya mwisho imebadilishwa: 21 Septemba, 2009 - Imetolewa 22:00 GMT
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
Mapigano ya kikabila yaua mamia Sudan
 

 
 
Kijana wa kabila la Lou Nuer kusini mwa Sudan akichunga ng'ombe
Makundi hasimu yanagombea mifugo, ardhi na rasilimali nyingine kusini mwa Sudan
Taarifa za jeshi la Sudan zinaeleza kundi la wanamgambo limewauwa zaidi ya watu 100 kusini mwa nchi hiyo katika mfululizo wa mapigano mapya yanayohusisha makabila.

Taarifa za Umoja wa Mataifa zimesema mamia ya watu waliokuwa na silaha kutoka kabila la Lou Nuer liliwashambulia raia pamoja na vikosi vya usalama katika kijiji cha Duk Padiet jimbo la Jonglei.

Mwezi uliopita kwenye jimbo hilo hilo watu wanaofikia 185 wa kabila la Lou Nuers waliuawa na waliposhambuliwa na wapiganaji wa kabila jingine la Murle.

Mwaka huu peke yake watu wanaofikia 2,000 wamekwisha kufa katika mashambulio yanayofanana na hayo kusini mwa Sudan.

Taarifa za awali kuhusiana na shambulio hilo la siku ya Jumapili katika kijiji hicho zilieleza idadi ndogo ya watu waliouawa.

Meja Jemedari Kuol Diem Kuol ameiambia BBC kwamba sehemu ya wapiganaji kutoka kundi la Sudan People's Liberation Army (SPLA) wamefanikiwa kukikomboa kijiji hicho.

Amesema wavamizi waliwalenga wanajeshi na kati ya waliouawa 22 ni wanajeshi akiwemo afisa wa cheo cha Meja.

Jemedari huyo amesema mashambulio hayo sio wizi wa mifugo bali ni ya kuwalenga wanajeshi.

Umoja wa Mataifa nchini Sudan umesema unafahamu kuhusiana na mashambulio hayo, lakini kwa sasa hauna taarifa za kina.

Chini ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005 kumaliza miongo miwili ya vita baina ya kaskazini na kusini mwa Sudan, waasi wa zamani wa kusini waliunda serikali ya kugawana madaraka na chama cha Rais Omar al-Bashir.

 
 
HABARI MPYA
 
 
Mtumie rafiki barua pepe   Chapisha
 
  Idhaa Yetu | Wasiliana Nasi
 
BBC Copyright Logo ^^ Rejea Juu
 
  Habari | Hali Ya Hewa
 
  BBC News >> | BBC Sport >> | BBC Weather >> | BBC World Service >> | BBC Languages >>
 
  Msaada | Wasiliana nasi | Maelezo ya Faragha