Sita wakamtwa kutaka 'kumuua' Karzai

Maafisa wa ujasusi wa Afghanistan wamesema wamewamakata watu sita waliokuwa wakipanga kumuua rais Hamid Karzai.

Watu hao wanatuhumiwa kupanga njama hizo walimshawishi mmoja wa walinzi wa Bw Karzai, maafis awamesema.

Waliokamatwa wametajwa kuhusika na kundi la wanamgambo la Haqqani, maafisa wamewaambia waandishi wa habari.

Wanagmabo wameuwa watu mashuhuri kadhaa nchini Afghanistan, katika miezi ya hivi karibuni.

"Kundi hatari na lenye watu wenye elimu, wakiwemo walimu na wanafunzi walitaka kumuua Rais Hamid Karzai". amesema msemaji wa shirika la ujasuzi la Afghanistan (NDS) Lutfullah Mashal.