Chakula kupungua duniani

Chakula Haki miliki ya picha UNIAN
Image caption Chakula

Umoja wa Mataifa unasema bei ya chakula huenda ikaendelea kuongezeka na kusababisha upungufu wa chakula duniani.

Katika ripoti yake ya kila mwaka mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa FAO,WFP,IFAD yameonya kuwa nchi ndogo zinazotegemea kuagiza chakula kutoka nje, hasa katika bara la Afrika zinakabiliwa na tishio hilo.

Yanasema kuongezeka kwa bei ya chakula ni changamoto ambazo zinahitaji juhudi zaidi kuafikia malengo ya maendeleo ya Milenia, ya kupunguza kwa nusu idadi ya watu wanaosumbuka kwa njaa kufikia mwaka 2015.

Thailand muuzaji mkubwa wa mchele duniani katika nchi za nje, imeonya kuwa zao lake la mpunga huenda likapungua kwa asili mia 15 mwaka huu kutokana na mafuriko na kuongezeka bei ya zao hilo.