Walinda amani Darfur wauawa

Imebadilishwa: 11 Oktoba, 2011 - Imetolewa 18:13 GMT


Wanajeshi watatu wa kulinda amani wameshambuliwa na kuuawa katika eneo la Darfur Kaskazini nchini Sudan, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Arfrika umesema katika taarifa yake.

Wanajeshi hao kutoka jeshi la pamoja na UN na AU - Unamid - walikuwa wakifanya doria katika kambi wa Zam Zam katika viunga vya mji wa Fasher.

Mhambuliaji mmoja pia alikufa, imesema taarifa hiyo. Walinda usalama sita walijeruhiwa, watau wakiumia sana.

Mkuu wa Unamid, Ibrahim Gambari amesema shambulio hilo ni "uhalifu wa kivita".

Amesema doria za Unamid ni jambo la "kawaida usiku na polisi wasio na silaha na wanajeshi wanaowasindikiza.

Lengo lao ni kulinda raia." amesema Bw Gambari.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.