Wapita njia wampuuza mtoto China

Kumekuwa na malalamiko nchini China baada ya kituo kimoja cha televisheni kuonyesha picha za watu wakipita tu na kumwacha mtoto mdogo akiwa barabarani baada ya kugongwa na gari.

Mtoto huyo wa miaka miwili yuko katika hali mbaya baada ya kugongwa sokoni kusini mwa mji wa Foshan.

Maelfu ya watu wanaotumia intaneti wameonyesha kukasirishwa na watu hao waliokuwa wakipita bila kumsaidia.

Wengine wanahisi watu hao walikuwa na wasiwasi wa kupewa jukumu la kulipa gharama za hospitali.