Berlusconi aponea chupuchupu

Waziri Mkuu wa Italia, Silvio Berlusconi, ameponea chupuchupu kura ya imani katika Bunge la nchio hiyo.

Chama chake cha ushirika wa mrengo wa kati- kulia ulishinda kura 316 dhidi ya kura 301.

Mwandishi wa BBC mjini Roma anasema kuwa kura hizo 316 ndio kiwango cha chini ambacho Bw Berlusconi alihitaji kusalia madarakani-- nusu ya viti bungeni.

Mwandishi wetu anaona kuwa ni ushindi finyu na unaiweka serikali ya ushirika kuongoza kwa udhaifu.

Viongozi wa upinzani waliitisha kura ya imani kutokana na jinsi matatizo ya kiuchumi yalivyosimamiwa pamoja na kashfa zilizoyakumba maisha binafsi ya Bw Berlusoni.