Kesi ya ubakaji ya Strauss-Kahn yafutwa

Uchunguzi wa madai ya ubakaji dhidi ya kiongozi wa zamani wa IMF, Dominique Strauss-Kahn umetupiliwa mbali.

Ofisi ya mwendesha mashtaka imesema ushahidi ulionesha kushambuliwa kijinsia - kosa ambalo si kubwa ikilinganishwa na kutaka kufanya ubakaji.

Mwandishi wa vitabu Tristane Banon alimtuhumu Bw Strauss-Kahn kutaka kumbaka mwaka 2003.

Tuhuma hizo zilizuka wakati Bw Strauss-Kahn akiwa anatuhumiwa mjini New York Marekani kwa ubakaji, tuhuma ambazo pia zilitupiliwa mbali.

Chini ya sheria za Ufaransa, kosa la kuutaka kubaka ni jela miaka 10, lakini miaka mitatu kwa kushambulia kijinsia.