Afisa wa UN aonyesha shaka kuhusu Syria

Afisa wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa ameyataka Mataifa ya kigeni yachukue hatua za dharura na kwa pamoja yajitahidi kuwalinda raia wa Syria dhidi ya hatua za serikali ya Syria.

Kamishna anayehusika na haki za bianadamu, Navi Pillay, amesema kua wakuu wa Syria wamekuwa wakitumia mbinu za kikatili dhidi ya waandamanaji wanaoipinga serikali,na kuongezea kua hali hio inatishia kuielekeza nchi katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Bi Pillay amesema kua zaidi ya watu elfu tatu wameuawa tangu mwezi machi. Matamshi yake yanatokea wakati wanaharakati wametangaza vifo vya takriban waandamanaji sita kwenye maandamano yaliyofanywa baada ya sala ya Ijumaa.