EU kutoa majibu ya janga la Ulaya

Mkutano wa Umoja wa Ulaya baadaye mwezi huu utakubaliana hatua "muhimu" za kupambana na janga la deni la Ulaya, amesema waziri wa fedha wa Ufaransa.

Mkutano huo utatoa "majibu kamili", amesema Francois Baroin mwishoni mwa mazunguzo baina ya mawaziri kutoka nchi za G20mjini Paris.

Amesema benku kuu "zitaendelea kuzisaidia benki nyingine".

Taarifa ya G20 pia imesema mawaziri "wamedhamiria kuwa IMF lazima iwe na rasilimali zenye uhakika".

Mkutano wa G20 umekuja huku kukiwa na wasiwasi kuhusu matatizo yanayohusiana na deni la Ulaya yakiendelea kusambaa.