Bi Clinton atembelea Libya bila taarifa

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi Hillary Clinton yupo Libya katika ziara ambayo haikutangazwa kwa nia ya kuonyesha kuwaunga mkono watu wa Libya na kujenga ushirikiano.

Bi Clinton anatarajiwa kuwepo mji mkuu, Tripoli, kwa saa chache. Ni afisa wa kwanza mwandamizi wa Marekani kutembelea nchi hiyo.

Ziara yake ilifanywa siri kutokana na sababu za kiusalama na hatua nzito za kiusalama zilifanyika kabla ya kuwasili kwake.

Kutembelea kwake mjini Libya kumefanyika baada ya ziara ya viongozi wa Uingereza na Ufaransa.