Wafanyakazi wailalamikia Malaysia

Serikali ya Malaysia imesema itaimarisha maeneo ya kufanyia kazi kwa wafanyakazi wa ndani kutoka nchi za kigeni.

Hatua hiyo imefanyika kufuatia madai kutoka serikali ya Cambodia kuwa wanawake wanaofanya kazi za ndani hudhalilishwa na waajiri wao wa Malaysia.

Baadhi ya wafanyakazi wa ndani wa Cambodia wamelalamika kupigwa na kubakwa.

Wiki iliyopita serikali ya Cambodia ilitoa kizuizi cha muda kwa wanawake wa Cambodia wanaofanya kazi za ndani Malaysia.