Waziri mkuu wa zamani wa Rwanda arejea

Aliyekuwa waziri mkuu wa Rwanda Pierre Celestin Rwigema amerejea nchini humo kutoka uhamishoni nchini Marekani .

Rwigema alikimbilia Marekani mwaka 2000 baada ya kujiuzulu kama waziri mkuu na kuwa mpinzani wa utawala wa Rais Paul Kagame.

Amerejea nchini Rwanda miezi michache baada ya serikali ya nchi hiyo kumuondoa kwenye orodha ya watuhumiwa wa mauaji ya kimbari kwa kuwa hakuna na ushahidi wa kutosha kuhusu mashtaka dhidi yake.

Licha ya kwamba alihudumu kwa muda wa miaka 5 kama waziri mkuu,hakuwa maarufu sana katika nyanja za kisiasa nchini Rwanda.