Watu 12 wauawa na bomu Afghanistan

Takriban watu 12 wameuawa na zaidi ya 30 kujeruhiwa katika shambulio la bomu kwenye tangi la mafuta.

Shambulio hilo limetokea katika kituo cha majeshi ya NATO huko Bagram, kaskazini mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Gavana wa jimbo la Parwan alisema watu wa eneo hilo walikimbilia mahala hapo wakiwa na ndoo ili kuchota mafuta yaliyokuwa yakitiririka kutoka tundu lililopasuka kwenye tangi hilo kutokana na bomu hilo.

Dakika chache baadae tangi hilo lililipuka, na kuua na kujeruhi wengi waliokuwa eneo hilo.