Israel na Misri wabadilishana wafungwa

Maafisa wa Misri wamekusanyika kwenye mpaka wa Israel kupokea wafungwa 25 wa Misri waliokuwa kwenye magereza ya Israeli.

Katika kubadilishana, Misri itamwachia huru mtu mmoja mwenye asili ya Kimarekani na Israeli ambaye anashutumiwa kwa ujasusi.

Israel ilisema Wamisri wengi wanajihusisha na magendo- si kwenye uhalifu wa kiusalama.

Mwisraeli-Mmarekani huyo, Ilan Grapel, alikamatwa Juni na kushutumiwa kwa ujasusi, lakini ushahidi mdogo sana ulipatikana dhidi yake.