Pakistan 'yaunga mkono' Taliban

Ushahidi mpya umeibuka, ukipendekeza kuwa Pakistan unaliunga mkono kundi la Taliban linalopigana na majeshi ya Marekani nchini Afghanistan.

Kamanda wa Taliban ameiambia BBC majeshi ya Pakistan yalihusishwa katika kuwapa mafunzo wapiganaji wa kitaliban.

Amesema majeshi hayo yanayotoa mafunzo yakiwa yamevaa sare za shirika la kijasusi la Pakistan, ISI, huwasili kila asubuhi kuwapa mafunzo maalum ya kutumia silaha.

Na aliyekuwa afisa wa shirika la kijasusi la kimarekani amesema mashambulio yaliyofanywa kwa ndege zisizo na rubani za Marekani kwa viongozi wa wapiganaji waliopo Pakistan yalifanikiwa tu pale Marekani ilipoacha kutoa tahadhari kabla kwa maafisa wa Pakistan.