Akutwa hai siku tano baada ya tetemeko

Kijana wa miaka 13 ameokolewa akiwa hai kutoka kwenye kifusi kusini mashariki mwa Uturuki, saa 108 baada ya tetemeko la ardhi nchini humo.

Kijana huyo aliyejeruhiwa aliokolewa kutoka kwenye jengo lilibomoka mjini Ercis.

Mapema saa chache tu mtu mwingine aliokolewa katika jengo lingine na kupelekwa hospitali.

Utawala wa Uturuki sasa unasema watu 570 wamekufa katika tetemeko hilo lililotokea Jumapili lenye kipimo cha 7.2- huku wengine zaidi ya 2,500 kujeruhiwa.