UNESCO kuamua juu ya Palestina

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mojawapo wa mikutano ya wanachama wa UNESCO katika vikao vyake siku zilizopita.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughukia utamaduni na sayansi- UNESCO linapiga kura leo mjini Paris kuamua iwapo litaikubali Palestina kama mwanachama kamili.

Hatua ya Palestina kushinikiza uanachama kamili wa shirika hilo ni sehemu ya kampeni ya kidiplomasia ya kutaka kukubalika kama mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa hatua inayopingwa vikali na Israeli na Marekani.

Iwapo UNESCO itakubali Palestina kuwa mwanachama wake kamili, basi Marekani inatishia kutumia sheria na kuondoa dola milioni sabini inazotoa kama mchango wake kwa UNESCO kila mwaka.

Marekani imeahidi pia kutumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi ujao wakati wa kura ya kuamua uanachama wa Palestina kwa Umoja wa Mataifa.