Italia yakabiliana na msukosuko wa fedha

Waziri mkuu mpya wa Italia Bw Mario Monti amewasilisha mipango yake ya kukabiliana na matatizo ya uchumi nchini mwake na pia kupunguza deni la nchi hiyo.

Hispania imo chini ya shinikizo kutoka kwenye masoko ya hisa kutokana na mzozo unaoendelea wa nchi zinazotumia sarafu ya Euro.

Viongozi wa muungano wa nchi za kusini mashariki mwa Asia wanaokutana nchini Indonesia, wamekubliana kuipa Burma nafasi ya kuwa mwenyekiti wa muungano huo mwaka 2014.

Rais Obama amesema Burma imeanza mazungumzo ya mabadiliko lakini inahitaji kufanya juhudi zaidi katika suala la haki za binadamu.