Mchekeshaji wa Nigeria aachiwa huru

Mahakama moja Nigeria imeamuru mchekeshaji maarufu Babu Suwe- aliyetiwa kizuizini kwa kushukiwa kufanya biashara haramu ya dawa za kulevya-aachiliwe kwa dhamana ifikapo Ijumaa.

Muigizaji na mchekeshaji huo alikamtwa Oktoba 12 baada ya kifaa cha ukaguzi wa mwili kwenye uwanja wa ndege wa Lagos kushuku kuwepo kwa dawa za kulevya ndani ya tumbo lake.

Wakili wake alisema kuendelea kwa hatua ya kutiwa kizuizini ni kinyume cha sheria.

Mashabiki na waigizaji wengine walikusanyika nje ya mahakama kuu mjini Lagos kuonyesha kumwuunga mkono mchekeshaji huyo wa Nigeria.