Assange huenda akarudishwa Sweden

Mwasisi wa wavuti wa wikileaks, Julian Assange, amepoteza kesi dhidi ya kuhamishwa kutoka Uingereza na kukabidhiwa Sweden, ambako anakabiliwa na mashtaka ya dhuluma za ngono na ubakaji.

Kufuatia uamuzi huo wa mahakama, Assange sasa huenda akasafirishwa kutoka Uingereza katika muda wa siku kumi zijazo.

Hata hivyo waandishi wa habari wanasema kuwa mawakili wake wanapanga kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama ya juu ya Uingereza.

Assange amekanusha madai hayo na kusema yamechochewa kisiasa.