Shutuma za ubaguzi wa rangi Ghana

Maafisa wa polisi nchini Ghana wanachunguza malalamiko ya ubaguzi wa rangi dhidi ya mmiliki wa mkahawa mmoja nchini humo.

Mwanamke wa Ghana, Elizabeth Okoro, amesema aliambiwa kuwa mkahawa huo kwa jina, the Atlantic Lobsters and Dolphin, katika mji mkuu Accra, unaruhusu wazungu pekee.

Mwenye mkahawa huo Marco Ranaldi hajakanusha kutoa matamshi hayo lakini amejitetea kuwa aliyatamka kama mzaha tu.

Bibi Okoro alianza kampeni ya kupiga vita hatua hiyo kwenye mitandao ya kijamii na kuvutia wafuasi wengi.

Kwa sasa mkahawa huo umefungwa na maafisa wa polisi wakidai ni ukiukaji wa sheria zinazoratibu utalii.