Rais Paul Biya aanza muhula wake wa 6

Mmoja wa viongozi ambao wamekuwa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, Paul Biya, wa Cameroon ameapishwa tena kuwa rais wa nchi hiyo katika sherehe iliyofanyika katika mji mkuu , Yaounde.

Bwana Biya ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka wa 1982 anaanza muhula wake wa sita na anatarajiwa kuongoza taifa hilo katika kipindi cha miaka saba ijayo kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

Biya alishinda uchaguzi mkuu wa urais mwezi uliopita ambao vyama vya upinzani pamoja na nchi za Ufaransa na Marekani zilisema kuwa uiligubikwa na dosari nyingi.