Wanne wafa, mkasa wa mgodi Uchina

Watu wanne wamefariki dunia na wengine 57 kukwama katika mgodi wa makaa ya mawe ulioporomoka katikati mwa Uchina.

Watu 75 walikuwa wanafanya kazi katika mgodi huo wakati wa mkasa ulipotokea.

Kumi na wanne kati yao walinusurika ajali hiyo lakini wengi wao wamekwama katika mgodi huo.

Shughuli za kuwatafuta manusura waliokwama katika mgodi huo zinaendelea.