Watu watano wauawa na polisi Tanzania

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, kaskazini magharibi mwa Tanzania limewaua watu watano wanaosadikiwa kuwa majambazi baada ya kurushiana risasi wakati watu hao walipojaribu kuiba katika duka moja katika barabara ya Nyerere kati kati ya jiji la Mwanza. Tukio hilo la kurushiana risasi limetokea mapema leo wakati watu hao wanaoasadikiwa kuwa majambazi, wakiwa na bunduki, bastola na mapanga kadhaa walipoingia katika duka hilo.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza ameiambia BBC kwamba majambazi hao walimwamuru mhudumu wa duka hilo kulala chini na kisha wakafanikiwa kuiba Shilingi 60,000 za Tanzania.