Kesi dhidi ya Carlos the Jackal yaanza Paris

Mwanamgambo wa kimataifa mwenye siasa za msimamo mkali, Carlos the Jackal, amefunguliwa mashtaka mjini Paris kuhusiana na shambulio la bomu dhidi ya treni moja nchini Ufaransa miaka ya themanini, lililosababisha vifo vya watu 11.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Carlos the Jackal

Carlos ambaye jina lake rasmi ni Ilich Ramirez Sanchez, tayari anatumikia kifungo cha maisha gerezani nchini humo, baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya maafisa wawili wa polisi.

Calos the Jackal, alikamatwa na wanajeshi wa Ufaransa nchini Sudan mwaka wa 1994.

Carlos, amekana mashtaka hayo, anawakilishwa na wakili wake ambaye pia alimuakilisha katika kesi ya kwanza, mwanamke ambaye alimuoa akiwa kizuizini.