Jenerali ashinda uchaguzi Guatemala

Aliyekuwa mkuu wa majesji nchini Guatemala Jenerali Otto Perez Molina, ameshinda uchaguzi wa urais ulioandaliwa nchini humo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais Mteule wa Guatemala Otto Perez Molina,

Baada ya takriban kura zote kuhesabiwa tume ya uchaguzi nchini humo imemtangaza Generali Otto Perez Molina, kuwa mshindi kwa kuzoa karibu asilimia 55 ya kura hizo.

Mpinzani wake, Manuel Baldizon, ambaye ni mfanyibiashara alipata asilimia 45.

Bwana Perez Molina atakuwa afisa wa kwanza wa zamani katika jeshi kuongoza taifa hilo tangu kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo mwaka 1996.

Aliahidi kuchukuwa hatua kali dhidi ya uhalifu na magenge ya ulanguzi wa dawa za kulevya kutoka mexico ambayo yako nchini Guatemala.