Wafanyakazi wa umma wagoma Israel

Wafanyakazi wa umma nchini Israel, wamefanya mgomo mfupi na kusababaisha hospitali kadhaa na ofisi za serikali kufungwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Benjamin Netanyahu

Shughuli za usafiri pia zilitatizika kwa muda nchini humo wakati wa mgumo huo uliodumu kwa muda wa masaa manne.

Kwa mujibu wa uamuzi uliotolewa na mahakama ya kitaifa ya wafanyakazi, mgomo huo utadumu kwa muda wa masaa manne pekee, baada ya mazungumzo kati ya chama cha wafanyakazi cha Histadrut na wizara ya fedha kusambaratika.

Chama hicho kinataka maelfu ya wafanyakazi wa kutoa huduma za usafi, walinzi na wafanyakazi wengine walioajiriwa na serikali ya nchi hiyo kupewa kandarasi ya kudumu.

Chama hicho kinataka serikali ya nchi hiyo kuongeza mishahara ya wafanyakazi hao mbali ya kuimarisha mazingira ya utendaji kazi.