Uvuvi haramu umekithiri nchini Libya.

Kuna ushahidi wa shughuli za uvuvi haramu katika Pwani ya Libya kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Image caption Pwani ya Libya

Taarifa zinasema meli za uvuvi hasa kutoka Bara Ulaya zilitumia ukosefu wa usalama nchini Libya kuvua aina ya papa adimu wa Samawati au Blue Tuna.

Bahari ya Mediterenian, karibu na ufukwe wa Libya, inaaminiwa kuwa na utajiri mkubwa wa samaki aina ya Blue fin.

Lakini hakukutarajiwa uvuvi wowote kufanyika katika eneo hilo, kwani serikali ya Libya, haikuafikia mahitaji ya kimataifa ya kuwa na uchunguzi wa nje kwa uvuvi huo.

Takwimu zilizotolewa na wachunguzi wa uvuvi huo, zimeonyesha kuwepo kwa wavuvi wengi katika maji ya Libya.