Upinzani umesema Homs ni eneo la hatari

Baraza la upinzani nchini Syria limetangaza mji wa Homs kuwa eneo hatari na kuomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Taarifa ya upinzani inasema majeshi ya serikali yamelenga maeneo ya makaazi kwa maroketi huku chakula na dawa zikiwa adimu.

Duru kutoka Homs zinasema kwamba maafisa wa usalama wameingia eneo la Baba Amr ambalo lilishuhudia makabiliano makali kati ya majeshi yaliyoasi na yale tiifu kwa serikali.