Serikali mpya kuundwa Ugiriki

Mawaziri nchini Ugiriki wameanza mkutano wa dharura kuzungumzia kuhusu kubuniwa kwa serikali mpya ya muungano wa kitaifa.

Kabla ya mkutano huo, chama kikuu cha upinzani kimesema lazima waziri mkuu mpya achaguliwe mara moja na kinatarajiwa tangazo hivi karibuni.

Serikali hiyo ya muungano itakayobuniwa inatarajiwa kutekeleza mpango mkali zaidi wa kubana matumizi ya pesa za umma kama mojawapo ya masharti ya kupewa mkopo utakaoisaidia Ugiriki kukabiliana na madeni yake makubwa.