Wasiwasi kuhusu uchaguzi nchini Liberia

Raia wa Liberia wanashiriki katika duru ya pili ya uchaguzi wa kiti cha urais.

Rais aliyepo madarakani Ellen Johnson Sirleaf alipata asilimia arobaini na nne ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.

Mpinzani wake Winston Tubman amesusia uchaguzi huo akisema serikali imekataa kushughulikia dosari zilizoshuhudiwa katika duru ya kwanza ya kura hizo. Wafuasi wake waliokabiliana vikali na polisi hapo jana wameitishia kuvuruga kura za leo.

Uhalali wa mchakato huu uko katika hali ya wasiwasi, ikiwa watakaopiga kura watakuwa wachache, Bi Sirleaf ambaye hivi majuzi alishinda tuzo ya amani ya Nobel, ataongoza nchi iliyogawanyika.