Serikali mpya kuzinduliwa leo-Ugiriki

Afisa wa serikali nchini Ugiriki amesema kuwa mpangilio wa serikali mpya ya muungano wa kitaifa itakayoshugulikia mgogoro wa kifedha unaokumba taifa hilo utatangazwa leo.

Afisa huyo amesema kuwa waziri mkuu, George Papandreou, ambaye tayari ametangaza kuwa atajiuzulu, atamtembelea rais wa taifa hilo kabla ya tangazo kutolewa.

Mazungumzo kati ya viongozi wa chama yalianza siku ya jumatatu.

Ripoti zilikuwa zimeashiria kwamba aliyekuwa makamu wa rais wa benki kuu ya umoja wa ulaya, Lucas Papademos, huenda akateuliwa kuwa waziri mkuu mpya lakini kuna taarifa kwamba mzozo umeibuka kuhusu uteuzi wake.