Serikali kusaidia waathiriwa wa mafuriko

Waziri mkuu wa Thailand, Yingluck Shinawatra, amependekeza kuwa serikali yake itatenga $4b zitakazotumika kwa shughuli ya kukarabati maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko tangu mwezi Julai mwaka huu.

Waziri huyo mkuu alitoa tangazo hilo, mbele ya bunge la nchi hiyo kama sehemu ya bajeti yake ya kila mwaka.

Kiongozi wa Upinzani nchini humo, Abhisit Vejjajiva, amesema kiasi hicho cha dola milioni nne hazitoshi.

Vejjajiva ametoa wito kwa waziri huyo mkuu, kutotimiza ahadi zake za kampeini, ili fedha zaidi zitumiwe kwa shughuli hiyo ya ukarabati kufuatia mafuriko mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa Thailand.