Mkutano wa APEC kuanza Hawii

Mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde, amesema anaamini kuwa Italia na Ugiriki zimepiga hatua kubwa katika harakati za kurejesha hali ya uthabiti na kutekeleza sera muhimu za kiuchumi ambazo shirika hilo la IMF na masoko ya kimataifa inahitaji.

Bi Lagarde aliyasema hayo nchini Japan, huku viongozi wa serikali wa mataifa ya kanda ya Asia na Pacific wakijiandaa kwa mkutano wao wa kila mwaka wa APEC mjini Hawii nchini Marekani.

Viongozi hao wa serikali wanatarajiwa kujadili mbinu za kukabiliana na matatizo ya kiuchumi duniani na hasa jinsi ya kulinda kanda hiyo kutokana na msuko suko unaoshuhudiwa barani Ulaya.

Mwandishi wa BBC, anasema Marekani inahisi kuwa mataifa ya Asia ni muhimu katika hatma ya siku zijazo kiuchumi na pia katika masuala ya ushirikiano wa kimataifa.