Bunge kujadili mageuzi ya kiuchumi Italia

Bunge la wawakilishi nchini Italia leo linatarajiwa kujadili mpango uliocheleweshwa wa mageuzi ya kiuchumi ambayo yananuiwa kusaidia kupunguza madeni ya serikali ya nchi hiyo.

Bunge la senate nchini humo liliidhinisha mageuzi hayo hapo jana.

Ikiwa mageuzi hayo yataidhinishwa na bunge hilo, waziri mkuu wa nchi hiyo Silvio Berlusconi, atalazimika kujiuzulu na aliyekuwa kamishna wa muungano wa Ulaya, Mario Monti kuchukua mahala pake.

Bei ya hisa iliimarika hapo jana baada ya bunge la senate kuidhinisha mageuzi hayo.

Imani katika masoko ya fedha pia iliongezeka kufautia kuapishwa kwa waziri mkuu mpya wa Ugiriki, Lucas Papademos.