Vatican kufadhili utafiti wa sayansi

Papa Mtakatifu Benedict wa 16 leo anatarajiwa kukutana na wanachama wa kampuni moja ya Marekani, NeoStem, ambayo inafanya utafiti kuhusu chembe chembe za mwili.

Makao makuu ya papa mtakatifu ya Vatican itawekeza dola milioni moja katika kipindi cha miaka mitano iajyo katika utafiti huo na mapema wiki hii iliandaa mkutano wa siku tatu kuhusu utafiti huo wa chembe chembe za mwili.

Kanisa la katoliki, linaunga mkono utafiti huo kama njia moja ya kutibu magonjwa.

Lakini kanisa hilo limepinga utafiti wa kiinitete, ikisema inakiuka maadili ya kijamii.