Wakereketwa wataka uwazi katika misaada

Wito umetolewa wa kuwepo kwa uwazi zaidi katika utoaji wa misaada.

Misaada ya maendeleo ya kimataifa inakadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 150.

Kundi la wakereketwa wa misaada hiyo lenye makao yake nchini Uingereza lijulikanalo kama ''Publish What You Fund'' linasema walipa kodi katika mataifa tajiri wanaotoa misaada na mtaifa maskini wapokeaji wa misaada wanahitaji taarifa zaidi ili kuelewa kama misaada hiyo inatumiwa ipaswavyo.

Kundi hilo limechapisha kielelezo cha misaada kadri inavyotolewa na mashirika katika nchi wahisani .