Wazee 2,000 wapewa usalama Kabul

Maafisa wa usalama wamewekwa katika hali ya tahadhari katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, kabla ya kongamano la wazee na viongozi 2,000 maarufu kama Loya Jirga.

Kongamano hilo liliitishwa na Hamid Karzai kujadili maridhiano na makundi ya waasi na uwezekano wa kuanzisha ushirikiano kati ya Afghanistan na Marekani.

Rais Karzai amewambia wajumbe katika mkutano wa Baraza la Viongozi wa kidini au Jirga kuwa atatoa maelezo zaidi juu ya maeneo mengine yanayopangwa kukabidhiwa kwa Serikali yake na shirika la Nato.