Waandamanaji watimuliwe New York, Jaji

Jaji mmoja mjini New York amepinga juhudi za waandamanaji wanaopinga ubepari waliotaka kuanzisha upya kambi ya malalamishi yao katika Wilaya moja ya kibiashara, baada ya kutimuliwa mnamo Jumanne.

Jaji aliamua kuwa ingawa waandamanaji wana uhuru kurudi katika bustani walikokuwa wakifanyia maandamano, utawala wa mji wa New York haujakiuka haki yao ya kutoa maoni kwa kutowaruhusu kufanya maandamano usiku kucha.

Waandamanaji walikuwa wamelalamika kwamba utawala wa New York ulipaswa kupata kibali cha mahakama kabla ya kuwatimua kwenye bustani hiyo, ambako walipiga kambi tangu kati ya Septemba.

Mjini London, utawala wa mji unapaswa kutoa ilani ya kisheria kwa waandamanaji waliopiga kambi nje ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Paul kabla ya kuwatimua.