Ukatili wa Khmer Rouge

Ushahidi wa kutisha umetolewa katika kesi ya uhalifu wa kivita uliofanyika nchini Cambodia mnamo miaka ya sabini.

Mwendesha mashtaka mwenza ameelezea mateso yaliyowakumba wafungwa, wengi wao wakikatwa mapua yao na vifaa vyenye makali, mtoto mmoja kufungwa kwenye mti na kupigwa hadi kufa, miongoni mwa visa vingine.

Mahakama maalum inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imewashtaki Nuon Chea, Ieng Sary na Khieu Samphan waliokuwa viongozi wa serikali ya Khmer Rouge kwa tuhuma za mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.

Takriban raia milioni mbili wa Cambodia walikufa kutokana na njaa na kunyanyaswa wakati wa utawala huo wa kiimla.