Kiwango cha Gesi chafu chaongezeka

Kiwango cha gesi ambazo huathiri mazingira kimeongezeka kufikia viwango hatari.

Haya ni kwa mjibu wa ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la utabiri wa hali anga duniani.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa kiwango cha gesi inayochafua mazingira ambayo inachangia pakubwa katika ongezeko la joto duniani imeongezeka kwa asilimia thelathini na tisa tangu miaka ya kwanza ya uzalishaji mkubwa wa bidhaa viwandani.

Shirika hilo linalaumu harakati za binadamu kuchoma mafuta asili, kutumia mbolea na kukata miti kuwa sababu kuu ya kuongezeka kwa gesi hiyo