Mtuhumiwa wa mauaji ya Cambodia ajitetea

Mmojawepo wa viongozi wa utawala wa Khmer Rouge nchini Cambodia ambaye yuko hai amejitetea dhidi ya tuhuma za mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu.

Nuon Chea amesema iwapo watawala wa sera za kikomunisti za kiimla wangeliwahurumia wasaliti nchi yao ingetokomea.

Hata hivyo amedai huenda maafisa wadhalimu katika utawala huo ndio waliohusika na mauaji ya watu milioni mbili katika miaka ya sabini.

Waendesha mashtaka katika mahakama maalum inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa wanasisitiza kwamba Bw. Chea na washtakiwa wenza wawili wanafaa kulaumiwa kwa ukatili huo.