Mgogoro wa chakula waikumba dunia

Umoja wa Mataifa umesema takwimu mpya zinaonyesha kuwa robo ya ardhi kwa sasa imeshuka thamani kwa kiwango kikubwa.

Kushuka huko kunaiweka dunia katika hali ya kukabiliwa na mgogoro wa chakula.

Umoja huo umepiga mahesabu kuwa wakulima wanahitaji kuzalisha zaidi ya asilimia sabini ya chakula ikifapo 2050 ili kukidhi mahitaji ya idadi ya watu wanaoongezeka duniani.

Lakini wamesema kuna kila dalili kuwa malengo hayo hayatofikiwa kutokana na kukosa njia bora za uzalishaji chakula na mabadiliko ya hali ya hewa.