Mjane wa Mitterrand afariki dunia

Danielle Mitterrand, mjane wa aliyekuwa rais wa Ufaransa, Francois Mitterrand, amefariki dunia katika hospitali moja nchini humo akiwa na umri wa miaka 87.

Bi. Mitterand alikuwa mwanaharakati wa ukombozi wa Ufaransa wakati wa vita ambaye baadaye alitumia wadhifa wake kama mke wa Rais kushinikiza haki za kibanadamu, kuunga mkono waasi wa ki-marx nchini El Salvador na kutetea haki za jamii ndogo ndogo kama vile wa-Kurdi na wa-Tibet.

Ofisi ya Rais Nicolas Sarkozy imemuomboleza kwa kumtaja kama mtu aliyewapa sauti wanyonge.