Raia Iran wavamia ubalozi wa Uingereza

Waandamanaji katika mji mkuu wa Iran, Tehran, wameingia kwa nguvu katika uwanja wa jengo la ubalozi wa Uingereza, wakilalamikia vikwazo vilivyowekwa na Uingereza dhidi ya Iran.

Televisheni ya Iran imeonyesha waandamanaji wakichana bendera ya Uingereza na pia wakitupa na kurusha nyaraka.

Taarifa zinasema kuwa sasa polisi wamelidhibiti eneo hilo.

Ofisi ya wizara ya mambo ya nchi za nje ya Uingereza imesema imekasirishwa sana na tukio hilo na kuilamu serikali ya Iran kwa kushindwa kuulinda ubalozi huo.