Muigizaji Clooney kufika mahakamani?

Mahakama ya Italia imetoa uamuzi kuwa muigizaji wa Hollywood George Clooney huenda akaitwa kama shahidi katika kesi ya aliyekuwa waziri mkuu, Silvio Berlusconi.

Anashutumiwa kulipia ngono kwa kahaba mwenye umri mdogo kulingana na sheria.

Mwanamke huyo ajulikanaye kwa jina la Ruby, alisema Bw Clooney alikuwepo kwenye chakula cha jioni alichohudhuria- japo amekana kuwepo.

Kuna orodha ya watu takriban 200 wanaodhaniwa kuwa mashahidi akiwemo mcheza soka wa timu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo- japo si wote watatokea mahakamani.