Ocampo awasili nchini Libya

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya jinai, Luis Moreno-Ocampo, amewasili nchini Libya kujadiliana na mamlaka nchini humo hatma ya Saif al Islam Gaddafi aliyekamatwa wiki iliyopita.

Saif al-Islam Gaddafi anasakwa na mahakama hiyo kwa tuhuma za uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo mauaji na mateso ya raia.

Mamlaka nchini Libya wanataka kumfungulia mashtaka nchini humo.

Bw. Moreno-Ocampo amesema majaji katika mahakama hiyo wataamua iwapo kesi hiyo itasikika nchini Libya ama katika mahakama ya kimataifa.