Umoja wa Mataifa yaishutumu Syria

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeishutumu Syria kwa kukiuka haki za binadamu kwa namna ambavyo imepambana na maandamano ya kuipinga serikali ya hivi karibuni.

Taarifa hiyo inadai kuwa mateso, udhalilishaji wa kijinsia, na kutoweka kwa watu ulikuwa ukitumiwa na serikali hiyo na majeshi ya usalama dhidi ya waandamanaji.

Wakati huo huo, Waziri wa mambo ya nje wa Syria Walid al-Moallem amesema uamuzi wa jumuiya ya nchi za kiarabu wa kuweka vikwazo dhidi ya nchi yake unainyima fursa nchi hiyo ya kutatua mgogoro uliopo.

Bw al-Moallem amesema jumuiya hiyo imekataa kukiri kuwepo wapiganaji wenye silaha nchini Syria.