Ujumbe wa Afghanistan wawasili Pakistan

Ujumbe wa Afghanistan unaochunguza mauaji ya rais wa zamani wa Afghanistan na mwenyekiti wa baraza kuu la amani nchini humo, Burhanudin Rabbani, umewasili nchini Pakistan katika ziara ya kikazi ya siku mbili kutafuta ukweli kuhusu mauaji ya kiongozi huyo.

Bwana Rabbani aliuawa mapema mwaka huu nyumbani kwake mjini Kabul na mshambuliaji wa kujitoa mhanga ambaye alificha bomu katika kilemba chake.