Afisa wa kukabiliana na ufisadi Nigeria aondolewa

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, amemuachisha kazi mkuu wa shirika la kupambana na ufisadi nchini humo.

Maelezo ya hatua hiyo ya Rais kumutimua Farida Waziri hayajatolewa.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamelishutumu shirika hilo kwamba halitekelezi kazi yake ipasavyo na linashinikizwa na wanasiasa kutenda kazi yake.

Aliyekuwa mkuu wa shirika hilo kabla ya Bi. Waziri, Nuhu Ribadu naye alilazimika kuachia wadhifa huo mwaka 2007.

Nigeria imekumbwa na visa vya ubadhirifu wa mali ya umma huku utajiri wa nchi hiyo ukitumia na maafisa wakuu kujitajirisha binafsi tangu kugunduliwa kwa mafuta ghafi katika miaka ya sabini.

Naibu wa Bi. Waziri, Ibrahim Lamorde ameteuliwa katika nafasi hiyo.